Call Us 0700 351 091

Near Kondele National Petrol Station Opposite Blood Bank, Off Nyerere RoadTom Mboya - Kisumu, Kenya


Je, wananchi wezangu mpo? Nina amani kuwa, nyinyi mko wazima kama garange za mvule. Mimi nipo mzima pia Rabuka amenitunza si haba.

Ningependa kuchukwa fursa hii kuwaeleza mengi kuhusu maendeleo ya jopo la Kiswahili katika skuli hii kwa yakini tumepiga hatua kubwa sana tangu mwaka juzi hadi sasa.

Kwa kweli tumekuwa pia tukikumbwa na changamoto si haba. Kumbuka hapa ni Kisumu, lugha ni kama adui wa waja. Lakini tunajaribu kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kuwas Kiswahili safi kimenenwa.

Wazazi wapenzi ningependa kuwaambia kuwa tusaidiane ili tuweze kuwahimiza wanafunzi wafanye vyem katika somo hili takatifu.

Sitamsahau mkurugenze pamoja na meneja kwa msaada wao wa kuwa somo hili linafanya vyema

Waama, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Tuungane pamoja tuwasaidie wanafunzi wetu. Sian mengi, Mola amwagie neema na Baraka teletele si ndogondogo.


Nawavulia kofia si haba. Ahsanteni.


Come join us in the race to excellence